Home BIASHARA Safari za Harare, Lusaka kuanza karibuni

Safari za Harare, Lusaka kuanza karibuni

0 comment 190 views

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi amesema ndege ya Airbus A220-300 inatarajia kuanza safari zake mpya kuelekea Harare (Zimbabwe) na Lusaka (Zambia) siku za hivi karibuni ambapo inatarajiwa kuwa zitafanyika mara tatu kwa wiki siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumapili.

“Sisi tutakuwa tunakwenda moja kwa moja hivyo tutakuwa tunatumia muda mchache sana angani, tutafika haraka, wateja wetu hawatapata usumbufu wa kwenda Afrika Kusini halafu ndo waende Harare au Lusaka kama wengine wanavyofanya”. Amesema Matindi.

Hadi sasa, Shirika la ATCL lina jumla ya ndege sita zikiwemo Bombardier Q400-8 tatu, Airbus A220-300 mbili pamoja na Boeing 787-8 (Dreamliner) moja. Ndege hizo zinafanya safari za nje kutoka Dar es salaam kwenda Comoro, Rwanda, Uganda, Burundi. Baadhi ya safari ya hapa ndani ya nchi ni kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es salaam kuelekea mikoa ya Mbeya, Bukoba, Dodoma, Mwanza, Kigoma, Kilimanjaro, Mtwara, Zanzibar, Tabora na Songea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter