Home KILIMO UNDP kufadhili mradi wa mboga

UNDP kufadhili mradi wa mboga

0 comment 111 views

Shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa (UNDP) limewafadhili wakulima 60 wa vijiji vya Huzi na Chifukulo wilaya ya Chamwino jijini Dodoma ili waweze kufanya kilimo cha mboga mboga. Ofisa Maendeleo Wilaya ya Chamwino, Sophia Swai amesema kuwa mradi huo ambao utatumia Milioni 60 umewalenga wakulima wadogo ili waweze kuboresha maisha yao na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakulima hao walipata fursa ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Fred Mwenemile ambae analima nyanya kwa kumwagilia kwa matone ambapo wamejifunza kuwa kilimo cha umwagiliaji kina faida zaidi na hivyo wanategemea kufanya aina ya kilimo hicho ili waweze kujikwamua kimaisha. Kwa upande wake Fred Mwenemile, amesema kilimo cha umwagiliaji kinamuhakikishia mkulima mavuno,  na kulingana na soko mkulima anapata faida na kuendelea kiuchumi.

Hata hivyo, Ofisa Kilimo wa wilaya ya Chamwino, Grace Nyamwanyi, amesema kilimo cha matone kina manufaa makubwa kwa  wakulima hao ambao wataweza kulima kilimo hicho huku wakiendelea na shughuli zao hivyo kujishughulisha na aina nyingine ya chanzo cha kupijatia fedha.

“Umwagiliaji huu ni mzuri hutumii nguvu, unafungulia maji unaendelea na shughuli zako baada ya muda uliopanga kumwagilia kuisha unafunga bomba unaendelea na shughuli nyingine”. Amesema Ofisa huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter