Home BIASHARA Wananchi kujipatia ng’ombe wa maziwa 396

Wananchi kujipatia ng’ombe wa maziwa 396

0 comment 155 views

Wananchi wa kata ya Igamba wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe, wamejipatia ng’ombe wa maziwa 396  kutoka Shirika la Heifer International Tanzania ambalo pia limetoa msaada wa kiwanda cha kuchakata vyakula vya mifugo. Kupitia mradi wake wa maziwa shirika hilo limetoa ng’ombe hizo ili kuwasaidia wakazi hao kujiinua kiuchumi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika hilo, Rose Marando, amesema kuwa wanawapa wananchi ng’ombe jike ili pale zitakapozalishwa ngombe nyingine jike basi wale ambao hawakupata awamu ya kwanza nah ii ya pili waweze kupata.

“Kupitia kauli mbiu yetu ya ‘toa zawadi kwa mwingine kila aliyepewa zawadi  awali anatakiwa na yeye atoe zawadi kwa mwingine ili kila mtu apate tunatamani huu utaratibu uende kizazi hadi kizazi  na pengine wilaya nzima wapate ng’ombe” amesema Marando

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kupitia ng’ombe hao wananchi watapata maziwa kwa ajili ya matumizi binafsi na kwa ajili ya kuyauza,pia watapata mbolea ambayo itatumika katika mashamba na hivyo kuleta maendeleo kwa wananchi hao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Plingo, alipokua akikabidhi ng’ombe 75 wa awamu ya pili amewataka wananchi hao kuwapa matunzo stahiki ng’ombe hao na pale ng’ombe atakapokufa kwa uzembe basi mwananchi husika atalipia.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter