Home BENKI Benki zaombwa kutoa mikopo kwa wakulima wadogo

Benki zaombwa kutoa mikopo kwa wakulima wadogo

0 comment 85 views
Na Mwandishi wetu

Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ameomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kusaidia wakulima wadogo wa ufuta na mihogo kwa kuwapatia mikopo ili wakulima hao wafanye kilimo cha kisasa na cha biashara. Zambi amesema hayo katika mkutano wa wadau wa korosho na ufuta mkoani huko uliofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Zambi amedai wakulima wadogo katika mkoa wake wapo tayari kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo ila wanakumbana na changamoto kubwa ya mitaji na hivyo wanashindwa kulima kisasa zaidi ili kukabiliana na ushindani katika soko la ndani na nje.

Ameongeza kuwa TADB ina wajibu wa kutoa mikopo ya riba nafuu ili wakulima waongeze uzalishaji na kujikwamua na janga la umaskini.Hivyo benki hiyo ikiboresha huduma za mikopo, wakulima wataweza kufikia uchumi wa kati kama serikali inavyotarajia.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TADB Francis Assenga amesema benki hiyo ina utayari wa kuwekeza katika miradi ya maendeleo ya kilimo na pia ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo walioko katika vikundi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter