Home KILIMO Vijana wasisitizwa kilimo

Vijana wasisitizwa kilimo

0 comment 140 views

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Stella Ikupa ametoa wito kwa vijana hapa nchini kujikita katika kilimo na kutumia vitalu nyumba kujifunza kilimo chenye tija ambacho kitawaunua kiuchumi na kuachana na dhana kuwa kilimo hufanywa na wazee. Naibu Waziri Ikupa amesema hayo wilayani Maswa mkoani Simiyu na kueleza kuwa, vijana wanatakiwa kuachana na imani kuwa kilimo kinapaswa kufanywa na wazee huku akiwataka kutumia nafasi hiyo kujifunza na kuwa mabalozi wa kilimo katika jamii zinazowazunguka.

“Kilimo kinaweza kuwatoa vijana kutoka mahali fulani kikawapeleka mahali pengine tena wakawa na uwezo mzuri kifedha kuliko hata wale walioajiriwa katika kazi za maofisini, niwashauri vijana muione fursa kupitia vitalu nyumba ondoeni dhana kwamba eti kilimo ni kazi ya wazee si kweli”. Ameshauri Ikupa.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri zao, vijana wana nafasi ya kupata mikopo na kuwasisitiza kuchangamkia fursa hiyo ili kuendeleza miradi yao ya uzalishaji, ikiwemo vitalu nyumba.

Baadhi ya vijana wanaojihusisha na utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba katika Kata ya Sola, wameipongeza serikali na kuomba jitihada zaidi zifanyike ili kuwafikia vijana wengi zaidi.

“Mimi ninaishukuru serikali yetu kwa kutuletea mradi wa kitalu nyumba, tumeshajifunza namna ya kutengeneza vitalu nyumba, kilimo bora chenye tija kupitia mradi huu, tunaomba mradi upelekwe mpaka ngazi ya kata ili vijana wengi waweze kunufaika  zaidi”. Amesema mmoja wao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter