Home FEDHAMIKOPO AfDB yaahidi mikopo

AfDB yaahidi mikopo

0 comment 101 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Dk. Mpango amesema hayo baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa benki hiyo, Dk. Akinwumi Adesina.

Waziri huyo amesema Rais wa AfDB amekubali ombi la Rais Magufuli la kuipatia Tanzania mkopo nafuu ili kuwezesha kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Msalato jijini Dodoma.

“Benki hii imekuwa ni ya msaada mkubwa sana na yapo maeneo mengi ambayo Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika amekubali kuendelea kushirikiana na nchi yetu”. Amesema Dk. Mpango.

Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema kuwa Dk. Adesina amepongeza jitihada za serikali katika kupiga vita rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa vitendo, kufanya maamuzi magumu ya kulinda rasilimali za taifa hasa madini, vilevile kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, kuimarisha ukusanyaji mapato na kudhibiti ukwepaji kodi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter