Home FEDHA Wananchi kulipwa mabilioni na Acacia

Wananchi kulipwa mabilioni na Acacia

0 comment 172 views

Meneja wa Idara ya Jamii Endelevu kutoka Mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Acacia North Mara, Richard Ojendo amesema mgodi huo unatarajia kuanza zoezi la kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi katika eneo la Nyamongo. Meneja huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa, Acacia inatarajia kulipa takribani Sh. 3.8 bilioni kwa zaidi ya wananchi 200 kutoka vijiji ambavyo vilifanyiwa tathmini mwaka 2011-12 na vilevile awamu za 35, 41 na 42 katika vijiji vya Nyabichune, Mjini kati, Nyangoto na Nyakunguru.

“Zoezi hili ni kwa wananchi halisi wa maeneo na awamu ambazo zimetajwa ambao taarifa zao zilichukuliwa na mgodi kwa ajili ya malipo ya fidia na orodha kamili wananchi watakaolipwa tayari tumekabidhi viongozi wa vijiji na vitongoji husika”. Ameeleza Ojendo.

Pamoja na hayo, Meneja huyo amesisitiza kuwa, malipo kwa awamu nyingine yataendelea kulipwa na wanufaika watapatiwa taarifa pale muda utakapofika. Aidha, Ojendo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mgodi huo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter