Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa amesema ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi – Kwamtoro – Singida utaanza muda wowote kuanzia sasa baada ya fedha za kuendesha mradi huo kupatikana. Naibu Waziri huyo amesema hayo Bungeni Dodoma na kuongeza kuwa barabara hiyo ni muhimu sana kwani inaunganisha ukanda wa mashariki, kaskazini, kati na magharibi. Vilevile amesema barabara hiyo inaunganisha mikoa iliyopitiwa na mradi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi mkoani Tanga hivyo ujenzi huo utasaidia kuinua uchumi kwa kiasi kikubwa.
Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa
Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...
Discussion about this post