Home BIASHARAUWEKEZAJI Windlab Kufanya Uwekezaji katika Miradi ya Maendeleo ya Afrika Mashariki

Windlab Kufanya Uwekezaji katika Miradi ya Maendeleo ya Afrika Mashariki

0 comment 67 views

Windlab Limited imetangaza makubaliano ya uwekezaji wa kiasi cha dola za kimarekani 10,000,000 na kampuni ya Eurus Energy Holdings Corporation (Eurus) katika miradi ya kibiashara ya Windlab East Africa. Windlab East Africa (WEA) inashikilia rasilimali za maendeleo ya miradi iliyopo katika kampuni hiyo pamoja na haki ya kutekeleza miradi ijayo katika nchi za Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundina Malawi.

Rasilimali za Windlab za Afrika Mashariki kwa sasa zinahusisha miradi ya maendeleo iliyoko katika mkakati ya utekelezaji yenye jumla ya takribani 1,650 MW ya uwezo unaotarajiwa, ambayo iko katika ngazi ya awali mpaka ngazi ya miradi iliyoidhinishwa. Mradi wa 300 MW wa Miombo Hewani Wind Farm nchini Tanzania, ambao umeorodheshwa katika orodha ya miradi inayofadhiliwa na serikali. Nchini Kenya, kampuni ya Windlab imeingia katika ushirikiano na serikali ya Mkoa wa Meru katika uendelezaji wa mradi wa nishati ya muunganiko ambao unajumuisha upepo, Jua na uhifadhi kwa njia ya betri mpaka kufikia uzalishaji wa 166 MW chini ya mpango wa PPP.

Windlab itatumia fedha hizi kuongeza kasi ya maendeleo ya miradi ya msingi Afrika Mashariki kukidhi mahitaji makubwa ya umeme ambayo hayajafikiwa. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Idadi ya watu walioko kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika kwa sasa inazidi watu 1 billioni na wanafurahia ukuaji wa kasi wa uchumi (GDP) duniani; Ethiopia asilimia8.2%, Kenya asilimia5.5%,na Tanzania asilimia6.8%.  Hata hivyo upatikanaji wa nishati ya umeme na uwezo wa uzalishaji wa nishati hiyo umebakia kuwa wa kiwango cha chini; kwa mfano, Tanzania ina idadi ya watu wapatao 59 millioni lakini ina kiasi cha 1,600 MW cha uzalishaji wa nishati.

Afrika mashariki ina vyanzo bora sana vya upepo, ambayo ni vyonzo vya msingi vinavyokamilisha misimu ya ukame, wakati ambapo mara nyingi sekta za nishati itokanayo na nguvu ya majiinapokuwa na changamoto ya uzalishaji. Kwa muingiliano wa sasa na wa hapo baadae wakikanda, sekta ya pamoja ya nishati ya umeme ni zao bora zaidi kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya udadi ya watu inayoongezeka.

“Tunafuraha sana kupata uungwaji mkono wa kampuni ya Eurus kama wadau katika WEA. Tutafanya kazi kwa pamoja kuharakisha maendeleo ya miradi yetu katika kanda hii. Wakati sehemu kubwa ya masoko haya hayakosi changamoto, mahitaji ya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya uzalishaji wa umeme uko wazi. Teknolojia ya uzalishaji wa umeme wa Upepo na Jua ni teknolojia yenye bei nafuu zaidi na uwekaji wake ni wa haraka zaidi na kutokana na hilo tunatarajia mahitaji mapya mengi zaidi yatafikiwa kwa kutumia nishati mbadala. Uwezo na uzoefu wa maendeleo wa kampuni ya WEA inaiweka katika nafasi nzuri kufanikisha fursa hizi.” Alisema bwana Roger Price, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Windlab.

“Eurus inafurahia uhusiano mwema na wa muda mrefu wa kiutendaji kati yao na Windlab ambao umekamilisha mradi wa nishati ya upepo wa Coonooer Bridge Wind Farm (Australia) na kufanya uboreshaji katika mradi wa Kennedy Energy Park hybrid project (Australia) wa pamoja.

Tunapongeza uwezo wao wa kiteknolojia wakubainisha na kujenga vyanzo bora zaidi vya nishati ya upepo na tunafuraha kupata fursa hii ya kuendeleza ushirikiano wetu na kufanya kazi pamoja katika masoko haya yanayochipukia.” Aliongeza bwana Hideyuki Inazumi,  Afisa Mtendaji Mkuu wa Eurus.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter