Home VIWANDA Kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea chazinduliwa

Kiwanda cha kuchakata taka kuwa mbolea chazinduliwa

0 comment 183 views

Kiwanda cha kuchakata na kuzigeuza taka kuwa mbolea halisi cha Mabwepande kilichojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6 ikiwa ni ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na Tanzania kupitia ushirikiano baina ya Jiji la Dar es salaam na Jiji la Hamburg kimezinduliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amezindua kiwand hicho na kusema kimekuja wakati muafaka ambao bei ya mbolea imepanda nchini.

Kupanda kwa bei ya mbolea kumetokana na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine ambapo ametoa wito kwa wananchi kununua mbolea hiyo.

Aidha RC Makalla amesema mkoa wa Dar es Salaam una uwezo wa kuzalisha zaidi ya Tani 23 za taka kwa siku hivyo kupatikana kwa kiwanda hicho itasaidia kuwa na uhakika wa mahala pa kuzipeleka.

RC Makalla ametoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusimamia vizuri uendeshaji wa kiwanda kwa kuhakikisha uzalishaji wa malighafi unakuwa wa kutosha.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema kuwa siku ya kesho Julai Mosi Meya wa Jiji la Hamburg na Meya wa Jiji la Dar es salaam wanataraji kuasini mkataba wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali.

Uzinduzi wa Kiwanda hicho umeshuhudiwa pia na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania na jopo la ujumbe wa wageni 46 kutoka Jiji la Hamburg nchini Ujerumani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter