Home KILIMO Mpango kuimarisha usambazaji mbegu, pembejeo wazinduliwa

Mpango kuimarisha usambazaji mbegu, pembejeo wazinduliwa

0 comment 116 views

Uzinduzi wa mpango wa kuimarisha mitandao ya usambazaji wa mbegu na viatilifu unaofanywa na mradi wa nafaka na kampuni ya kimataifa ya Corteva kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini umefanyika jana jijini Dar es salaam. Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mitandao hiyo iko imara kwa sababu asilimia 65 ya wananchi wanategemea ajira katika sekta ya kilimo. Waziri huyo amesema kuwa usambazaji wa mbegu na viatilifu utamhakikishia mkulima chakula na kipato.

Waziri Hasunga ameeleza kuwa hadi sasa serikali na wadau wa maendeleo wanaendelea kutekeleza programu ya miaka 10 ya ASDP II iliyoanza kufanyiwa kazi mwaka jana. Programu hiyo inagusa maeneo ya usimamizi endelevu wa maji na ardhi, kuongeza tija (matumizi ya pembejeo), kuongeza masoko na kuongeza thamani ya mazao, kuboresha mazingira ya uwekezaji katika kilimo ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta hiyo.

“Ni imani yangu kuwa kufanikiwa kwa kazi hii ya mradi wa nafaka ni kufanikiwa katika utekelezaji wa sehemu ya ASDP II. Mradi huu pia utaendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya serikali na sekta binafsi katika kuendeleza kilimo nchini”. Amesema Hasunga.

Aiddha, Waziri huyo ametoa shukrani kwa Shirika la misaada la kimarekani (USAID) kwa kuendelea kutoa ushirikano wake kwa serikali katika kuhakikisha sekta mbalimbali zinaendelea, hususani sekta ya Kilimo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter