Home BIASHARAUWEKEZAJI Parachichi ni ‘dhahabu ya kijani’

Parachichi ni ‘dhahabu ya kijani’

0 comment 201 views

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angellah Kairuki amesema zao la parachichi limegeuka kuwa ‘Dhahabu ya kijani’ kwa nchi za barani Afrika kutokana na uwekezaji wake kuinua uchumi katika nchi zinazozalisha kwa wingi.

“Ukiangalia kwa wenzetu wa Kenya, zao hilo limeyapita mazao mengine na limekuwa ni namba moja kuliko hata zao la chai na kahawa. Mapato yake ni makubwa sana, nadhani tunapaswa kuongeza nguvu kuvutia wawekezaji wengi zaidi na hasa ukizingatia kwamba zao hili la parachichi kwa sasa hivi wanaita dhahabu ya kijani”. Amesema Kairuki.

Waziri huyo amesisitiza kuwa serikali tatoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji wa zao hilo kutoka ndani na nje ya nchi kwa kuangalia aina ya vivutio ili kuwawezesha wawekezaji hao kufanya vizuri zaidi.

“Tunataka tuweze kupata ajira, tuweze kupata teknolojia mpya na za kisasa, lakini zaidi tuweze kukuza uchumi na pato la mwananchi wetu mmoja mmoja. Katika mkoa wa Kilimanjaro, wilaya ya Siha wamefanya vizuri sana katika maparachichi na Hai wameanza kufanya vizuri”. Ameeleza Waziri huyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter