Home BIASHARA Tanga Fresh wafunguka maziwa kukosa viwango

Tanga Fresh wafunguka maziwa kukosa viwango

0 comment 249 views

Katika ziara ya Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk katika kiwanda cha maziwa Tanga Fresh, Mbunge huyo ameelezwa kuwa moja ya changamoto kiwandani hapo ni maziwa yaliyo chini ya viwango kutoka kwa wafugaji.

Meneja Mkuu wa kiwanda hicho ambacho makao yake makuu ni Tanga, Michael Karata amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika lita 120,000 kwa siku lakini hadi sasa wanasindika lita 50,000 tu. Aidha, Meneja huyo amedai maziwa yanakuwa chini ya kiwango kutokana na wafugaji wengi kuchanganya maji kwenye maziwa na vilevile ng’ombe kukosa lishe bora kutokana na ukame, hali inayowapelekea ng’ombe hao kukosa afya bora.

“Mahitaji ya maziwa bado  ni makubwa sana. Tunahitaji maziwa bora na yenye viwango ili kushindana kwenye soko la kimataifa lakini kiwango kikubwa cha maziwa ya wafugaji wetu hayakidhi viwango na ubora unaohitajika”. Amesema Karata.

Kwa upande wake, Mbunge Mbarouk ametoa wito kwa wafugaji kuchangamkia soko la ndani na kumshauri muwekezaji huyo kutoa mikopo kwa wafugaji ili waweze kuzalisha zaidi na katika viwango stahiki.

“Nikuombe Karata utoe mikopo kwa wafugaji ili kuongeza uzalishaji wa maziwa bora maana wafugaji wengi wa Tanzania hawana vifaa na wengi wao ni wafugaji wa kuhama hama. Hii inapunguza uzalishaji wa maziwa bora”. Ameeleza Mbunge huyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter