Kampuni ya Vodacom imefanikiwa kutoa gawio la Sh.83.81 kwa kila mwanahisa wake baada ya kupata faida ya takribani Sh.170.24 bilioni kwa mwaka ulioishia Machi 31. Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Ian Ferrao amesema kampuni hiyo imefanikiwa kutengeneza faida kubwa katika maeneo matatu ambayo ni huduma, mauzo ya data pamoja na M-Pesa. Ferrao ameeleza kuwa wamepata mafanikio hayo kutokana na kuboresha huduma wanazotoa kwa wateja na kuimarika kwa matumizi ya data na mfumo wa fedha ambao unaboreshwa mara kwa mara.
Serikali, Benki ya Dunia wajadili ushiriki Sekta binafsi
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru amesema Serikali inafanya majadiliano ya kimkakati na Benki ya Dunia...
Discussion about this post