Home BIASHARA Nguo za ndani mitumba bado changamoto

Nguo za ndani mitumba bado changamoto

0 comment 124 views

Baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufanya ukaguzi wa kushtukiza sokoni Sido jijini Mbeya, imeelezwa kuwa wafanyabishara wasio waaminifu wameendelea kuingiza nguo za ndani za mitumba kupitia njia zisizo halali, hali ambayo inahatarisha afya za watumiaji. Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile amesema lengo la zoezi hilo ni kuhakikisha kuwa biashara ya nguo hizo za mitumba inakomeshwa na wananchi wanaacha kuzitumia kwani zinaweza kuleta madhara ikiwemo magonjwa ya ngozi.

Kufuatia operesheni hiyo ambayo ilikamata zaidi ya marobota 20, Andusamile amewaambia waandishi wa habari kuwa, wanatarajia kuteketeza nguo hizo wakishapata kibali kutoka Halmashauri ya jiji la Mbeya na kuongeza kwamba wataendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi.

Naye Mkaguzi Ubora wa shirika hilo kutoka Makao Makuu, Baraka Mbajije amesema wataziteketeza nguo hizo kwa sababu wafanyabiashara wameshindwa kutoa ushirikiano kwa TBS.

“Tunashindwa kabisa kuitokomeza biashara hii kwa sababu tukiwataka hawa wauzaji waeleze walikozinunua lakini hawatupi ushirikiano, ndio maana tunawanyang’anya na kuziteketeza, sasa hivi tunasubiri taratibu zikamilike, tutakuwa tunakamata wauzaji”. Amesema Mbajije.

Mmoja wa wahanga wa zoezi hilo, Given Sanga amesema nguo zilizochukuliwa zimegharimu takribani Sh. 10 milioni. Amewaomba wataalamu kuendelea kutoa elimu ili wafanyabiashara waepuke kupata hasara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter