Home BIASHARAUWEKEZAJI JPM ateta na Bogdanov, amshukuru Rais Putin

JPM ateta na Bogdanov, amshukuru Rais Putin

0 comment 102 views

Kufuatia mahusiano mazuri baina ya Tanzania na Urusi, Rais John Pombe Magufuli amekutana na wajumbe wa Urusi wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mikhail Bogdanov ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Urusi kuhusu masuala ya Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es salaam, Rais Magufuli ametoa shukrani zake za dhati kwa Rais Vladimir Putin kwa kuendelea kudumisha uhusiano mzuri na Tanzania huku akimhakikishia kuwa, serikali yake inatambua umuhimu wake na itaendelea kukuza mahusiano hayo kwenye biashara, uwekezaji, utalii na masuala ya kijamii.

“Naomba ufikishe ujumbe wangu kwa Rais Putin, watanzania wanaipenda Urusi na tunamkaribisha kuja kutembelea nchi yetu na wananchi wengine wa Urusi. Tunawakaribisha pia wawekezaji waje wawekeze katika fursa mbalimbali zilizopo hapa kwa kwa manufaa yetu sote”. Amesema Rais Magufuli.

Naye Bogdanov, amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake na kumhakikishia kuwa Urusi itaendelea kushiriki katika maendeleo ya Tanzania ikiwemo mpango wa kusaini makubaliano ya kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano (JPC) upande wa biashara, uwekezaji na uchumi ili pande zote ziweze kunufaika.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema kuwa kupitia JPC Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi .

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter