Home BIASHARA Changamoto mfumo mpya wa usajili BRELA

Changamoto mfumo mpya wa usajili BRELA

0 comment 115 views

Mfumo mpya wa usajili kwa njia ya mtandao wa Wakala Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umepelekea wafanyabiashara kupata ugumu katika kusajili biashara zao. Wakili Benedict Ishabakaki, kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amethibitisha uwepo wa changamoto hiyo na kuelezea kuwa mfumo huo ni mzuri hasa kutokana na kuleta muamko kwa wananchi wengi ambao wanataka kuwekeza.

Ishabakaki amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutatua changamoto hiyo ili kuendelea kuwavutia wafanyabiashara. Ametaja changamoto nyingine ambayo inahitaji kutatuliwa na uongozi ni baadhi ya wafanyakazi wa BRELA kuwapa ushirikiano mdogo wafanyabiashara pale wanapokuwa wanahitaji msaada kutoka kwao.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Emmanuel Kakwenzi, amesema kuna umuhimu wa kupata tathmini kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusu mfumo huo ulioanzishwa takribani mwaka mmoja uliopita.

“Tunataka kusikia kutoka kwa TLS wamepokea vipi mfumo huu mpya, kama ni kurekebisha turekebishe wapi na mafanikio ni yapi tuboreshe wapi zaidi”. Amesema Mtendaji huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter