Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mradi wa Ubungo Interchange waanza rasmi

Mradi wa Ubungo Interchange waanza rasmi

0 comment 112 views

Meneja wa Mradi wa Ubungo Interchange, Barakaeli Mmari amesema foleni za magari katika barabara za Morogoro na Sam Nujoma zimepungua baada ya ujenzi wa Ubungo Interchange kuanza rasmi. Mmari ameeleza kuwa kupitia ujenzi huo, tayari uzio wa mzunguko wa magari umeshatengenezwa, na kwa kiasi kikubwa umesaidia kupungua kwa foleni kwenye barabara hizo.

“Baada ya kumaliza kazi, ujenzi wa barabara za pembeni zinazosaidia magari kuchepuka ulianza na kazi yake sasa imefikia pazuri” Amesema Meneja huyo.

Mmari ameeleza kuwa hadi sasa, mchakato wa uainishaji na kuhamisha miundombinu umekamilika huku akitaja miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na umeme kilomita 17, gesi kilomita 1.2, maji kilomita 2.6 na simu kilomita 2.6.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale amesema mradi wa Terminal III  unaojengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 247 utakamilika Julai mwakani ambapo hadi sasa, nguzo 130 kati ya nguzo 576 tayari zimeshachimbwa ardhini kwenye daraja hilo la ngazi tatu. Mfugale ameongeza kuwa hadi kufikia Julai mwakani, barabara ya juu inayotoka Mwenge kwenda Bandarini itakuwa imeshakamilika huku barabara ya juu  inayotoka mjini hadi Kimara ikitarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu. Kuhusu daraja la Salendar, Mtendaji huyo amesema daraja la muda linategemea kukamilika Juni mwaka huu na daraja kubwa litaanza kujengwa baada ya daraja hilo la muda kukamilika.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter