Home BIASHARA Nyama hatarishi zateketezwa Arusha

Nyama hatarishi zateketezwa Arusha

0 comment 116 views

Operesheni Nzagamba imefanikisha kukamatwa na kuteketezwa kwa kilo 26,295 za nyama mbovu ya ng’ombe na nguruwe zenye viambata vya sumu jijini Arusha zilizoingizwa nchini pasipo kufuata kanuni na taratibu za Sheria. Waziri na Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema wafanyabiashara ambao wamekuwa wakipitisha bidhaa kiholela hawatapata nafasi hiyo tena kwani Wizara hiyo imeweka vizuizi ili kutokomeza biashara hiyo haramu.

“Hakuna muujiza ambao watautumia wa kuendelea na mchezo huu wa kuingiza nchini bidhaa za mifugo ambazo hazijakaguliwa, bila vibali, zilizokwisha muda wa matumizi, zinazokwepa kodi, hatutachoka kuwakamata na kutaifisha mali zao, hatutachoka kuwapiga faini na kuwapeleka mahakamani, hatutachoka kuendelea kuteketeza mitaji yao na kwamba ili kujiepusha na mgogoro na serikali nawasihi sana wafuate Sheria”. Amesema Waziri Mpina.

Aidha, Waziri huyo ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaokiuka Sheria na kuwataka watendaji wote waliopo mipakani mwa nchi kuhakikisha biashara zinafanyika kwa haki kwani serikali haijazuia uagizaji wa mifugo nje ya nchi.

“Watu hawa wachache wasitake kutumia uhalifu wao kwa ajili ya kuchonganisha uhusiano mzuri uliojengeka kwa muda mrefu baina yamataifa haya kwa kisingizio cha kuhusisha uhalifu wao na uhusiano wetu na kwamba wahalifu wataendelea kubeba misalaba yao wenyewe”. Ameeleza Waziri huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter