Home BIASHARAUWEKEZAJI Taasisi zaagizwa kushirikiana kuimarisha uwekezaji

Taasisi zaagizwa kushirikiana kuimarisha uwekezaji

0 comment 110 views

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amezitaka taasisi za serikali zinazoshughulika na mahitaji ya sekta ya uwekezaji kudumisha ushirikiano ili kuepuka vikwazo visivyo vya lazima ambavyo huwakatisha tamaa wanaokuja nchini kwa dhumuni la kuwekeza. Warioba ametoa ushauri huo wakati akifungua kikao kazi kilichoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mkoa wa Kilimanjaro. Baadhi ya taasisi zilizohudhuria kikao hicho ni pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Mamlaka ya Mapato (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Uhamiaji, Idara ya Kazi, Ardhi pamoja na Maofisa Biashara.

“Mkiacha ule urasimu wenu mnaotaka kunyenyekewa ili kutimiza wajibu wenu ambao uko kisheria, suala ya vikwazo au mwekezaji kulalamikia hili na lile mtakapotoa ushirikiano sekta ya uwekezaji itakuwa na mchango mkubwa kwa taifa. Urasimu hauna nafasi katika serikali hii, tuhakikishe wawekezaji wanapata mahitaji ya msingi ili wawekeze mitaji yao”. Ameekeza Mkuu huyo.

Warioba amezitaka taasisi hizo kutoa ushauri kwa serikali pale zinapoona inasababisha vikwazo katika utekelezaji wa masuala yanayohatarisha mazingira rafiki ya uwekezaji. Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kilimanjaro, Albert Rwelamira ameshauri wawekezaji kutoka nje ya nchi kuzingatia Sheria.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter