Home FEDHAHISA Unafahamu haya kuhusu hisa?

Unafahamu haya kuhusu hisa?

0 comment 118 views

Kampuni nyingi hususani taasisi za kifedha zimekuwa zikiwaalika wananchi kununua na kuwekeza kwenye hisa ili waweze kunufaika. Unaweza kujiuliza nini hasa ni faida ya kumiliki hisa?

Hisa ni kipande kinachoashiria wewe ni mmiliki wa sehemu ya kampuni fulani na endapo kama kampuni hiyo itatengeneza faida basi na wewe mnunuzi wa hisa utanufaika. Baadhi ya kampuni huuza hisa mara tu wakifungua biashara na wengine husubiri mpaka pale wanapotaka kupanua zaidi biashara. Ukiwa na idadi kubwa ya hisa katika kampuni, basi unakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi.

Kwa kawaida, mgao wa faida katika kampuni kati ya wanahisa hufanywa kila mwisho wa mwaka ambapo huwa kunakuwa na kikao ambacho lengo lake ni kujadili faida zilizopatikana katika kampuni na kama wanahisa wanataka waendelee kuwekeza katika kampuni hiyo au wanataka kugawana faida iliyopatikana.

Aina za Hisa:

Hisa za Waanzilishi

Aina hii ya hisa hupewa kwa waanzilishi ambao hawapewi mgao wa kila mwaka na badala yake, wanapata mgao pale faida katika kampuni ikiongezeka/ikizidi.

Hisa za Kampuni

Hii hutolewa kwa wafanyakazi katika kampuni, na mfanyakazi anaruhusiwa kununua hisa hiyo bila kikomo na hata pale atakapostaafu kazi.

Hisa za Wamiliki

Hisa hizi ni kwa wale wamiliki wa kampuni ambao kikawaida humiliki hisa kubwa, na wna kuwa na maamuzi kuhusu uendeshaji wa kampuni. Kukiwa na faida basi wamiliki wa hisa hii hufaidika zaidi, na kukiwa na  hasara wamiliki wa hisa hii hupoteza zaidi ya wanahisa wengine.

Hisa za Kawaida

Hisa hii humilikiwa na watu wa kawaida ambao mara nyingi huwa ndio kundi kubwa lakini kila mmoja wao anakuwa amenunua hisa ndogondogo. Wanahisa hawa hupata wakati mgumu pale kampuni inapopata hasara kuliko wamiliki wengine wa hisa.

Kwa upande wa kampuni, faida ya hisa ni uhakika wa mtaji. Watu wakinunua hisa basi kampuni hiyo inakuwa na uhakika wa mtaji hata pale hasara itakapotokea. Kwa upande wa wamiliki, hisa inaweza kukuletea faida au hasara. Unashauriwa kuwekeza idadi kubwa ya hisa ili uweze kunufaika zaidi.

Pia unapaswa kufahamu lengo lako wakati wa kununua hisa. Wengine hufanya hivyo kwa lengo la kuziuza pale zinapokuwa zimepanda bei au kufaidika na mgao mwishoni mwa mwaka au muda uliopangwa na kampuni husika.

Hapa nchini, masuala yote ya hisa yanashughulikiwa na Soko la Hisa Dar es salaam (DSE). Inashauriwa kuwa, kabla hujafanya maamuzi yoyote kuhusu uwekezaji wa aina hii, pata elimu zaidi kuhusu hisa ili uweze kufanya maamuzi sahihi ambayo yataleta manufaa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter