Home FEDHA Prof. Luoga atoa ufafanuzi usafirishaji dola

Prof. Luoga atoa ufafanuzi usafirishaji dola

0 comment 130 views

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga ameeleza wakati akifafanua kuhusu ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kuwa, masharti ya kusafirisha dola ni magumu katika kila nchi na sio Tanzania peke yake.

Prof. Luoga amesema kuwa masharti ya kusafirisha dola yamekuwepo tangu mwaka 1992 nchini na katika nchi nyingine ambapo fedha ambayo unaruhusiwa kutoka nayo nchini ni ile ambayo unaruhusiwa kuingia nayo katika nchi nyingine.

“Kwa mfano unaposafirisha dola kutoka Tanzania inategemea unazipeleka wapi. Marekani huruhusiwi kuingiza zaidi ya dola 10,000 na ukipeleka Uingereza nacho kuna kiwango hicho hicho ambacho huwezi kuruhusiwa kwenda nacho”. Ameeleza Gavana huyo.

Pia amesema kuwa Sheria hiyo inaweza kumpelekea mtu kuingiza fedha kinyume na Sheria kama anataka kuingiza kiasi kikubwa cha fedha nchi nyingine.

“Si kweli kwamba masharti ya Tanzania ni magumu bali masharti ya kila nchi unayokwenda ni magumu katika kubeba dola zako kupeleka kwako. Ukikutwa na dola 400,000 kwa mfano swali ni utaenda kuingiza vipi kwenye nchi unayokwenda? Ambayo haitakuruhusu kuingiza zaidi ya dola 10,000?”. Amesema Gavana huyo.

Kuhusu ukaguzi wa maduka ya kubadilishia fedha katika mikoa mingine, Prof. Luoga amesema wameshafanya ukaguzi na wamiliki ambao hawajakidhi masharti wameshapewa notisi kuwa watafungiwa.

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter