Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Ubalozi wa Kenya wapanda miti kumsherehekea Wangari Maathai

Ubalozi wa Kenya wapanda miti kumsherehekea Wangari Maathai

0 comment 104 views

Ubalozi wa Kenya, mabalozi wa nchi za Africa na wawakilishi kutoka sekta binafsi wamepanda miti ikiwa ni ishara ya kusherehekea maisha ya mwanaharakati wa mazingira, profesa Wangari Maathai leo katika tafrija fupi iliyofanyika katika ubalozi wa Kenya.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mh Dan Kazungu akipanda mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafriji fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania (3 kushoto) na wafanyakazi wa ubalozi huo wakipanda mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa Mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafriji fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa.

Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Norway na UNDP, Nancy Shedrack na Helge Flaard wakimwagilia mti kama ishara ya kumsherehekea Profesa Wangari Maathai, mwanaharakati wa mazingira kutoka Africa mashariki. Tukio hili limefanyika leo wakati wa tafriji fupi iliyoandaliwa na ubalozi wa Kenya na kuhudhuriwa na mabalozi mbalimbali wa nchi za Africa, wawakilishi kutoka sekta binafsi na Umoja wa Mataifa. Katikati ni Balozi wa Kenya, Mh Dan Kazungu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter