Home WANAWAKE NA MAENDELEO Access Bank, EIB zatoa elimu kwa wanawake

Access Bank, EIB zatoa elimu kwa wanawake

0 comment 139 views

Benki ya Access Tanzania Limited kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB), wametoa mafunzo ya msingi ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wanawake jijini Dar es salaam na kuanzisha akaunti ya “Lulu” kwa ajili ya kundi hilo. Ofisa biashara wa benki hiyo, Prosper William amesema jukwaa hilo la biashara ni la kwanza kufanyika kwa mwaka 2019  na benki hiyo, ukiachana na mengine yanayotegemea kufanyika katika mikoa mingine.

Kupitia jukwaa hilo, wanawake hao, wamiliki wa biashara ndogo, za kati na kubwa ambao ni wateja na wasio wateja wa benki hiyo wamepata ujuzi kuhusu usimamizi wa biashara zao, ulipaji wa kodi na kuweka mapato yao benki ili kukuza biashara zao. Ofisa huyo ameeleza kuwa lengo la benki  hiyo ni kuhakikisha kuwa wanawake wanafundishwa maadili ya biashara na utendaji, pamoja na kusaidiwa kujiwekea akiba kwa kasi kwa ajili ya siku zijazo.

Naye, Jennifer Bashwas wa EIB amesema kuna umuhimu wa kutumia benki kama chombo cha kujipatia mikopo au kuweka akiba ili kufikia malengo binafsi. Mafunzo hayo yamelenga kukuza uongozi mzuri na kazi ya timu katika biashara na maisha binafsi.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter