Home VIWANDAMIUNDOMBINU Kiongozi wa Mwenge agomea mradi

Kiongozi wa Mwenge agomea mradi

0 comment 126 views

Kiongozi wa Mwenge 2019, Mkongea Ali, amekataa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa zaidi ya Sh. 800 bilioni wa Itumba Isongole mkoani Mbeya baada ya kubaini kwamba nyaraka ya taarifa na ile inayoelezea ujenzi zinatofautiana. Kiongozi huyo amedai imeshindikana kuweka jiwe la msingi katika mradi huo ambao unategemea kuwanufaisha wananchi zaidi ya 3000 kutokana na upungufu huo kwani kwa taratibu zilizopo, lazima nyaraka maalum ambayo inaonyesha gharama zilizoongezeka kwenye mradi iandaliwe kwa sababu fedha zinazotumika ni za serikali.

“Mshauri wa mradi ni mtu muhimu sana sasa kwanini hayupo hapa wakati yeye ndiye mwakilishi wa serikali, nani atatupa maelekezo yanayoeleweka kama yeye hajajua umuhimu wake na umuhimu wa mbio za mwenge kwenye miradi ya serikali, pia kwanini msimamizi aliruhusu gharama kuongezeka kwenye mradi huu bila maelekezo au nyaraka yoyote inayoonyesha gharama kuongezeka”. Amehoji Kiongozi huyo

Aidha, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude kufuatilia suala hilo kwa kina akishirikiana na vyombo husika ili kujua ukweli wa mabadiliko hayo. Kwa Upande wake, Mhandisi  wa mradi huo, Abdallah Digelo, amebainisha kuwa mradi huo umechelewa kutokana na mabadiliko na maboresho waliyoyafanya kwenye tanki pamoja na usafi wa miundombinu katika eneo hilo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter