Home KILIMO Kampuni yajikita kuleta mageuzi kilimo cha chai

Kampuni yajikita kuleta mageuzi kilimo cha chai

0 comment 205 views

Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya DL Group, Dk. David Langat amesema kampuni hiyo imejenga ghala kubwa la kuhifadhia zao la chai litakalowasaidia wakulima kupunguza asilimia 50 ya gharama za usafirishaji wa zao hilo na kurahisisha upatikanaji wa masoko kupitia minada itakayoandaliwa. Dk. Langat ameeleza kuwa kampuni hiyo imelenga kushirikiana na serikali, pamoja na wakulima ili kukuza kilimo na biashara ya zao hilo.

“Moja ya mambo ambayo yamekuwa yakirudisha nyuma ulimaji na biashara ya chai Tanzania ni ukosefu wa ‘warehouse’ (ghala mahususi) kwa ajili ya kusimamia ufanyikaji  wa minada ya chai. Sasa tunajenga ghala hilo ili iwezekane kusimamia ufanyikaji wa minada hiyo maana kwa miaka 49 haukupata kufanyika mnada wa chai Tanzania. Kuwa na ghala ni hatua nzuri na muhimu”. Amesema Dk. Langat.

Pia ameeleza kuwa ghala hilo limeshathibitishwa na Chama cha Biashara ya Chai Afrika Mashariki (EATTA) kuwa ni mwanachama na wamepanga kufanya minada ya chai kutoka Tanzania, Rwanda, Burundi na Malawi jijini Dar es Salaam na chai hiyo itasafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Dar es salaam.

“Lengo letu ni pana, maana tunataka wakulima wapate bei nzuri, tuongeze zao la chai thamani na kuondoa kila aina ya adha inayokwamisha chai kuuzwa ng’ambo. Mafanikio katika juhudi hii yatachochea uuzaji wa chai nchi za nje”. Amesema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter