Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita amesema endapo Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) itawapatia kibali cha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo kazi, wanaweza kununua mabasi 100 ya mwendokasi na kuyaingiza barabarani. Mwita amesema hayo wakati akipokea Bodi ya Jiji la Kisumu kutoka nchini Kenya ambao wamekuja kupata elimu kuhusu mradi huo.
“Kwetu sisi kama jiji tuna fedha za kuendesha huo mradi na tunaamini hata kama hatutomaliza changamoto lakini tutasaidia kuondoa adha ya usafiri wanayopata wananchi. Pia niwaombe radhi wananchi ambao wanapata tabu na usafiri huo kwa kuwa hata jiji halifurahishwi ndio maana hata sisi tunataka tunataka tuingie katika biashara hiyo”. Amesema Mwita.
Mabli na hayo, Meya huyo amesema kuwa mradi huo ni wa kisasa ndio maana Bodi hiyo kutoka Kenya imekuja nchini ili kupata mafunzo kuhusu mradi huo. Ametumia nafasi hiyo kuhakikisha kuwa, watafanya jitihada zote kupunguza kero ya usafiri wanayokumbana nayo wakazi wa Dar es salaam.