Home BIASHARA Namanga yang’aa kibiashara

Namanga yang’aa kibiashara

0 comment 120 views

Meneja Msaidizi wa forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), mkoani Arusha Godfrey Kitundu amesema bidhaa za viwandani zinazouzwa nje ya nchi kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga (Arusha) zimeongezeka kutoka tani 21,478 hadi tani 26,690. Kitundu amesema hayo wakati akitoa tathmini ya Kituo cha Huduma cha Pamoja Mpakani (OSBP) Namanga, ikiwa ni mwaka mmoja na nusu tangu kuanzishwa kwake.

Kitundu ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17 kumekuwa na ongezeko la malori yanayosafirisha bidhaa kupitia mpaka huo ambapo awali, kulikuwa na malori 1,268 lakini kufikia Machi mwaka huu yameongezeka na kufika malori 1,585, hivyo kupunguza kero ya mizigo kusafirishwa kwa muda mrefu katika mpaka huo.

Mbali na hayo, Meneja huyo amesema idadi ya bidhaa zilizoongezwa thamani zimeongezeka kutoka 429 hadi 640 hadi mwaka jana. Ametaja bidhaa ambazo zinaongoza kuuzwa nje kuwa ni marumaru, vinywaji vya matunda na vya kuongeza nguvu, unga wa ngano na sembe, konyagi, playwood, marine boards, kraft liner, mbogamboga, matunda, mashudu ya pamba, tangawizi pamoja na madini ya viwandani.

“Thamani ya bidhaa zilizokamatwa zikiingia nchini pasipo kufuata taratibu zimepungua kutoka za zaidi ya Sh. milioni 630.3 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia bidhaa za zaidi ya Sh. milioni 24.7kwa mwaka 2017/18”. Amesema Kitundu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter