Home KILIMO Wakulima kupewa vitambulisho bure

Wakulima kupewa vitambulisho bure

0 comment 109 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema asilimia 72 ya wakulima wa mazao takribani nane ya biashara tayari wamesajiliwa ili kupata vitambulisho vya bure. Hasunga amesema hayo jijini Dodoma alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali ikiwamo ‘tablets’ 50 na kuongeza kuwa, Wizara ya Kilimo inalenga kutambua mazao wanayolima wakulima hao, ukubwa wake na vilevile mahali yalipo.

“Umefika wakati muafaka sasa mkulima kuwa na kitambulisho, kanzidata hii itaambatana na utoaji wa vitambulisho kwa wakulima ili watembee kifua mbele na ifikapo juni mwaka huu, zoezi hili litakuwa limekamilika ili tujue tuna wakulima wangapi kwenye mazao yetu”. Amesema Waziri Hasunga.

Ametaja mazao hayo kuwa ni pamoja na pamba, miwa, korosho, kahawa, chai, pareto, alizeti na michikichi ambapo hadi kufika Machi 31 mwaka huu, wakulima 1,274,337 walikuwa wameshasajiliwa. Hasunga ameeleza kuwa lengo la serikali ni kuwafikia wakulima  milioni 1.7 hivyo kuzitaka bodi za mazao kukamilisha hilo.

Hadi sasa Wizara hiyo imetambua uwepo wa mashamba makubwa 134 ya kahawa, pareto, mkonge, chai, pamba na korosho. Waziri Hasunga ametoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kutoa vifaa vya kukamilisha zoezi hilo la usajili wa wakulima nchini.

Naye Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Natalie Boucly amesema suala la uwekaji wa takwimu ni muhimu ndio maana wameona kuna umuhimu wa kutoa vifaa hivyo ili kuisaidia serikali kufanikisha kampeni hiyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter