Home FEDHAMIKOPO Halmashauri yatoa mamilioni

Halmashauri yatoa mamilioni

0 comment 114 views

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Nestory Dagharo amesema Halmashauri hiyo imetoa mikopo ya Sh. 40 milioni kwa vikundi 14 kutoka kata 10, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la Halmashauri zote nchini kutoa asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi maalum.

Dagharo ametoa wito kwa vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo kutumia fedha walizopata vizuri na kuwasisitiza kurejesha mikopo hiyo kwa muda uliopangwa ili kuwapa nafasi wengine wanaohitaji mikopo hiyo kuendeleza shughuli zao.

“Vikundi ni vingi ndani ya wilaya na wameomba mikopo ninyi mmebahatika, kafanyieni kazi na mkumbuke kurejesha”. Amesema Kaimu huyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Grace Mghase amesema katika vikundi 14 vilivyopatiwa mikopo, sita ni vya wanawake (Sh. 18.5 milioni), vitano vya vijana (Sh. 14 milioni) na vitatu ni vya watu wenye ulemavu (Sh. 8 milioni).

“Robo ya kwanza na ya pili tumetoa Sh. 92,630,000 na sasa robo ya tatu ya mwaka tunatoa Sh. 40 milioni”. Amesema Mghase.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter