Benki ya Stanbic Tanzania imeandaa jukwaa la kuwajengea ujuzi wateja wake katika fursa mbalimbali zilizopo katika kilimo cha biashara pamoja na utalii. Mafunzo hayo yalifanyika jijini Arusha yakiongozwa na Mtaalamu wa Uchumi kutoka Stanbic Bank, Jibran Quereishi.

Mtaalamu wa Uchumi kutoka Stanbic Bank, Jibran Quereishi akizungumza katika jukwaa la kujenga ujuzi kwa wateja lilioandaliwa na benki hiyo, kwa ajili ya kuwaonyesha wateja wake fursa mbali mbali zilizopo katika kilimo cha biashara pamoja na utalii, hivi karibuni mkoani Arusha. Benki ya Stanbic iliandaa jukwaa hilo ili kutekeleza ahadi ya kuwasaidia wateja wake kufikia mafanikio yao ya kifedha kwa kupitia fursa mbali mbali zilizopo katika sekta husika.