Home BIASHARA Smartphone zinazotamba kwa sasa

Smartphone zinazotamba kwa sasa

0 comment 87 views

Kila mwaka huwa kunakuwa na matoleo mapya ya simu aina ya Smartphone kutoka makampuni mbalimbali, lengo likiwa ni kuwateka wateja wa simu hizo.

Zifuatazo ni baadhi ya simu zinazotamba sokoni kwa sasa kumsaidia mnunuaji kufanya maamuzi sahihi:

Samsung Galaxy S10+

Simu hii imezinduliwa rasmi Machi mwaka huu. Ni simu nzuri ya aina yake. Simu hii ina kioo chenye ukubwa wa inchi 6.4, huku ikiwa na uwezo wa kufunga simu kwa kidole hivyo kumhakikishia mtumiaji usalama. Pia Samsung wamezidi kuboresha kamera zao ambapo katika simu hii, kuna kamera 5, mbili za mbele na tatu za nyuma. Kwenye upande wa betri, simu hii ina uwezo wa kukaa hadi siku mbili kulingana na matumizi ya mtumiaji, pia mtumiaji anaweza kuchaji simu hii bila chaja (Wireless). Samsung hii pia ni Dust na Waterproof.

Sifa:

  • Ukubwa wa kioo cha simu hii unaridhisha.
  • Finger Print ambayo haionekani inamuhakikishia mtumiaji usalama zaidi.
  • Uwezo wa kuchaji simu pasipo chaja (Wireless Charging).
  • Uhai wa betri.
  • Mtumiaji amepewa uhuru wa kuchagua aina ya kamera anayotaka.

Iphone Xs Max

Simu hii inasifika kwa kioo chache kikubwa cha inchi 6.5. Ilizinduliwa rasmi mwaka jana. Simu hii imetengenezwa kwa kioo mbele na nyuma na fremu isiyoshika kutu. Kamera yake pia ni kivutio kikubwa kinachofanya watu wavutiwe nayo. Pia ina betri ambayo hujaa chaji baada ya dakika 30. Chaji kwenye simu hii ina uwezo wa kukaa masaa 79 kulingana na matumizi. Inaweza kutumika ikiwa ndani ya maji.

Sifa:

  • Betri yake inakaa muda mrefu.
  • Kioo chake ni kikubwa hivyo mtumiaji anaona vitu vizuri, na kwa wanaopenda video na picha simu hii inafaa zaidi.
  • Ufanisi na spidi yake ni nzuri.
  • Maboresho katika uhimili wa maji (Waterproof).
  • Kamera yake ni nzuri.
  • Sio kawaida kwa simu za IOS kutumia laini mbili lakini simu hii inampa mtumiaji uwezo huu.

Huawei P30 Pro

Simu hii ni kati ya simu nzuri zilizotoka mwaka huu. Wadau wanasema simu hii na Samsung Galaxy s10+ zinakwenda sambamba. Ina kamera tatu za nyuma zenye MP 40 (wide), MP 20 (utra wide) na Periscope MP 8 huku kamera ya mbele ikiwa na Megapixel 32. Simu hii inasifika kwa loki ya kidole. Kwa upande wa betri, simu hii inachaji kwa haraka na pia inarudisha chaji inapoisha (reverse charging). Huawei wamebuni kadi za kumbukumbu maalumu kwa ajili ya kuweka vitu kama simu imejaa hivyo kadi za kumbukumbu za kawaida haziwezi kutumika kwenye simu hii.

Sifa:

  • Kamera yake inatoa picha nzuri sana.
  • Betri yake ina ufanisi mzuri na hukaa muda mrefu.
  • Ufanisi wake ni wa haraka hivyo mtumiaji hupata matokeo ndani ya muda mchache
  • Picha sehemu zisizokuwa na mwanga zinatoka vizuri sana.

Nokia 9 PureView

Toleo la kwanza la simu hii limetoka Februali mwaka huu. Nokia wamejikita katika soko la picha kwa kutoa simu hii kwani simu hii ina lensi tano zenye megapixel 12 kila moja ambazo hutumika kupiga picha moja. Mtumiaji wa simu hii ana uwezo wa kuitumia sehemu zenye vumbi na maji (hadi mita moja kwa dakika 30). Simu hii ina kioo chenye inchi 5.99. Sifa yake nyingine kubwa ni loki ya kidole inayoonekana. Vilevile, simu hii huingiza chaji haraka na inawezekana kuchaji bila chaja (Wireless).

Sifa:

  • Inatoa picha nzuri.
  • Haiuzwi bei kubwa sokoni.
  • Usalama wa simu kutokana na loki ya kidole.
  • Uwezo wa kutumia kwenye maji na vumbi.

Meizu 16s

Kati ya sifa kubwa ya simu hii ni kamera yake yenye megapixel 48 nyuma na megapixel 20 mbele. Ilitangazwa Aprili mwaka huu na ina uwezo wa kuweka laini mbili, ukubwa wa sehemu ya kumbukumbu unaweza kufika hadi GB 128. Pia kwa usalama, Meizu hii ina loki ya kidole. Betri yake pia inawahi kujaa.

Sifa:

  • Usalama wa simu kutokana na loki ya kidole.
  • Picha nzuri,
  • Sio ghali kama simu nyingine.

Simu hii imeanza kutolewa oda siku mbili zilizopita huko China, hivyo maoni zaidi yatapatikana baada ya watu kuitumia na kuizoea. Lakini hadi sasa, sifa zake zinahamasisha watumiaji.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter