Home KILIMO Wakulima walamba mabilioni

Wakulima walamba mabilioni

0 comment 98 views

Ofisa Kilimo wa Lindi, Majid Mayo amesema wakulima wa korosho mkoani humo wamelipwa kiasi cha Shilingi Bilioni 192.5 kufuatia mauzo ya korosho ghafi kilo milioni 58.5 kati ya kilo milioni 59.3. Mayo ameeleza hayo wakati wa kikao kilichowakutanisha wakuu wa wilaya, maofisa kilimo, wakurugenzi wa wilaya, vyama vya ushirika pamoja na wanunuzi. Ofisa Kilimo huyo ameongeza kuwa, licha ya makusanyo kuwa chini ikilinganishwa na msimu wa 2017/18 ambapo walikusanya kilo milioni 76, malipo hayo ni asilimia 98 ya kilo milioni 59.3 ambazo tayari zimeshapokelewa kwenye maghala makuu mkoani humo.

Ofisa huyo ameainisha mpangilio wa makusanyo ya kilo hizo kama ifuatavyo: Kilwa wakulima walikuwa 1,106 ambao walikuwa na kilo 1,500 kila mmoja waliohakikiwa kwa kilo milioni 2.7 na wakulima 9,345 wenye chini ya kilo 1,500 kila mmoja kwa kilo 3.7 jumla kukiwa na kilo 6.4. Wilaya ya Lindi vijijini kulikuwa na zaidi ya kilo 1,500 wakulima 1,624 wenye kilo milioni 3.2 na chini ya kilo 1,500 za wakulima 36,646 wenye kilo milioni 8.2 ambapo jumla ya kilo milioni 11.4 zimehakikiwa. Kwa upande wa Lindi Mjini, zaidi ya kilo 1,500 za wakulima 142 wenye kilo 293,811 zimehakikiwa huku chini ya kilo 1,500 za wakulima 5,095 wenye kilo milioni 1.1. Jumla wilaya hiyo ina kilo milioni 1.4. Wilayani Liwale zaidi ya kilo 1,500 zimehakikiwa kwa wakulima 1,404 wenye kilo milioni 2.5 na chini ya kilo 1500 zilikuwa  za wakulima 29,550 wenye kilo milioni 9.6 jumla zaidi ya kilo milioni 16.

Pamoja na hayo, baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho wamedai kutolipwa fedha zao kwa msimu wa mwaka huu hadi sasa.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter