Home BIASHARA Kwanini biashara yako inahitaji tovuti

Kwanini biashara yako inahitaji tovuti

0 comment 112 views

Kila biashara inahitaji kuwa na mpangilio maalum ili kufika mbali. Katika ulimwengu huu wa kidigitali, kuwa na biashara ni zaidi ya kumiliki ofisi au duka. Unahitaji pia kuwekeza kwenye teknolojia kwani ni soko ambalo lina watu wengi zaidi ambao unaweza unaweza kuwafikia kwa urahisi. Kama mfanyabiashara, umewahi kufikiria kuwa na tovuti? Unajua mchango mkubwa wa tovuti kwenye kukuza biashara yako?

Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini unatakiwa kufanya hivyo leo na kuanzisha tovuti kwa ajili ya biashara yako.

Hujenga uaminifu
Kwa sababu matumizi ya intaneti ni makubwa, watu wengi zaidi wamekuwa wakitumia mitandao mbalimbali kutafuta bidhaa badala ya kwenda madukani kama ilivyokuwa zamani. Ikiwa biashara yako itakuwa na tovuti, bai kuna uwezekano mkubwa kuwa itakuwa kwa kasi na kuaminika zaidi. Biashara isiyokua na tovuti hupelekea wateja kukosa taarifa muhimu wanazohitaji hivyo kukosa imani nayo. Endapo biashara yako ikiwa na tovuti, ni fursa nzuri ya kuwafikia watu wengi zaidi kwa urahisi na kupanua soko.

Gharama zake ni nafuu
Gharama za mfanyabiashara kumiliki tovuti ni nafuu kwani mara baada ya kukamilisha tovuti (bei hutofautiana), unapunguza gharama za kuweka matangazo magaeztini n.k. Aidha, upatikanaji wa soko kwa kupitia tovuti ni mkubwa zaidi kulinganisha na njia nyingine.

Inarahisisha kufuatilia wateja
Tovuti ni njia bora ya kuwawezesha wateja wako kufahamu uwepo wa bidhaa mpya, matukio yanayokuja, matangazo pamoja huduma zingine zingine unazotoa. Tovuti yako inaweza kutoa taarifa zilizopo kwenye biashara na ikawafikia watu wengi zaidi kwa gharama nafuu na ndani ya muda mfupi.

Hupatikana mahali na muda wowote
Tovuti hupatikana kwa wateja wako muda wowote hivyo inakuwa rahisi kwao kuchunguza na kuchagua bidhaa na huduma hata wakati ambapo duka au ofisi imefungwa. Hatua hii ina umuhimu mkubwa kwa mteja kwani humsaidia kuamua kununua au la.

Fursa ya kuwa na soko kubwa
Tovuti yako itatoa sehemu mbadala ya kuuza. Kama muuzaji, tovuti ina nafasi nzuri ya kuuza bidhaa zako kwenye soko pana na kubwa, pia huduma zinaweza kupatikana duniani kote.

Kuonyesha kazi/bidhaa
Bila kujali aina ni gani ya biashara unafanya, tovuti ni sehemu nzuri ya kuonyesha kazi yako kwa kuweka picha au hata ushuhuda kutoka kwa wateja. Unaweza kuonyesha nini kinachofanya biashara yako kuwa ya kipekee ukilinganisha na nyingine.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter