Home VIWANDAMIUNDOMBINU Bandari kavu, Suluhisho foleni Dar

Bandari kavu, Suluhisho foleni Dar

0 comment 117 views

Wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20 bungeni Dodoma, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby ameitaka serikali kujenga bandari kavu katika eneo la Vigwaza,Pwani ili kupunguza msongamano wa magari yanayotoka katika bandari ya Dar es Salaam.

“Mmoja wa watu ambaye nilikuwa situmii bandari ya Dar es Salaam ni mimi lakini katika miaka mitatu sasa natumia na wakati mwingine nawategeshea vitu loose ili nione kama vitaibiwa lakini iko vizuri sana na haina wizi na ina speed (kasi) ya hali ya juu sana” ameeleza Mbunge huyo, na kuongeza kuwa:

“Kwasababu ya uzuri wa bandari hiyo kumekuwa na malori mengi yanayopita katika barabara zetu. Sasa tulizungumza sana tuanzishe dry port (bandari kavu) ya pale Vigwaza ili malori yawe yanaishia pale na mizigo ichukuliwe na reli ambayo sasa yafanya kazi hadi Vigwaza” amesema.

Pia amesema kuwa gharama za kutoa mizigo bandarini ni nafuu na kupitisha mizigo kwa reli kutapunguza foleni jijini Dar es Salaam na  ajali za maroli na magari ya kawaida zitapungua.

Aidha, ameisisitizia serikali kutimiza ahadi ya kujenga barabara ya kati ya Kongwa na Mpwapwa.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter