Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji wafurahia udhibiti bidhaa za nje

Wawekezaji wafurahia udhibiti bidhaa za nje

0 comment 108 views

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekagua ujenzi wa kiwanda kipya cha nyama cha Eliya Foods Over Seas Limited kilichopo Longido na kiwanda cha Maziwa cha Kiimanjaro Fresh kilichopo Arusha ambapo wakati wa ukaguzi huo, wawekezaji wa viwanda hivyo wametoa shukrani kwa serikali kwa kudhibiti uingizaji holela wa nyama na maziwa kutoka nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Eliya Foods Over Seas Limited, Shabbir Virje ameeleza kuwa kufuatia udhibiti huo, wamepata msukumo mkubwa wa kuanzisha kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 500 na mbuzi 200 kwa siku huku kikiwa kimelenga kununua mifugo katika wilaya ya Longido na maeneo mengine na kutoa ajira kwa watanzania 200.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya Galaxy Food&Beverage Ltd ambao ni wazalishaji wa Kilimanjaro Fresh, Irfhan Virje amesema kampuni hiyo imehamasishwa kuanzisha kiwanda hicho kutokana na maamuzi ya serikali ya kuweka tozo mpya kwenye uagizaji wa bidhaa za maziwa kutoka nje ya nchi. Aidha amesema kutokana na uamuzi huo, wameweza kuzalisha maziwa kwa gharama nafuu na kuleta urahisi kwa watumiaji wa bidhaa hiyo.

kwa upande wake, Waziri Mpina amesisitiza kuwa serikali imejikita katika kudhibiti uingizaji holela wa bidhaa za mifugo na kuwatoa hofu wawekezaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter