Home VIWANDAMIUNDOMBINU WAPCOS yafadhili mradi wa maji

WAPCOS yafadhili mradi wa maji

0 comment 109 views

Kampuni ya WAPCOS Limited ya India imetoa shilingi bilioni 15.6 ambayo ni sawa na dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya mradi wa maji katika miji 29 nchini, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India kupitia benki ya Exim.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amethibitisha hilo na kueleza kuwa wizara hiyo imesaini mkataba na WAPCOS huku akifafanua kwa ufupi kuwa mkataba huo ni kwa ajili ya kuandaa taarifa ya kina kuhusu miradi yote ya miji hiyo  29.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inaeleza kuwa watu walioshiriki kutia saini katika mkataba huo wenye sehemu mbili ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo na Meneja Mkazi wa Kampuni ya WAPCOS Ltd Chandrasekhar Kombathula.

“Mkataba uliosainiwa ni hatua ya awali na inahusu kazi mbili ambazo ni kuandaa taarifa ya kina kuhusu miradi yote ya miji 29 ikiwamo maeneo maji yatakapopatikana na ya pili ikiwa ni kuandaa nyaraka za zabuni ili kuwapa wakandarasi watakaotekeleza mradi”.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter