Home VIWANDANISHATI Treni ya umeme kuendeshwa na Stiegler’s Gorge

Treni ya umeme kuendeshwa na Stiegler’s Gorge

0 comment 68 views

Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, ametangaza kuwa umeme wa mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge utatumika kuendeshea treni mpya ya umeme. Dk. Kalemani amesema hayo mkoani Morogoro alipokuwa kwenye kikao cha mawaziri na makatibu wakuu ambao wizara zao zinatekeleza mradi huo.

Kikao hicho kimekutanisha watalaamu na viongozi mbalimbali kati yao wakiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  January Makamba.

“Mradi huu utazalisha megawati 2,100 na ndio utakaotumika kuendeshea treni ya kisasa ya umeme ya Standard Gauge. Amesema Dk. Kalemani.

Katika kikao hicho, Dk. Kalemani amesema serikali itachukua hatua stahiki za kisheria kwa watakaokwamisha uwekezaji katika mradi huo unaohusisha wizara takribani 11. Mbali na hayo, taarifa kutoka kwa wataalamu kuhusu mradi huo zimejadiliwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter