Home KILIMO Mahindi kukatwa kodi

Mahindi kukatwa kodi

0 comment 118 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Kastori Msigala ametoa notisi inayofafanua uuzaji wa mahindi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), ambapo imeelezwa kuwa wakulima katika Halmashauri hiyo wanatakiwa kuuza mahindi yaliyovunwa katika msimu wa 2017/18 na katika mauzo hayo, watakatwa kodi ya zuio 2%.

“Bei elekezi iliyopitishwa ghalani ni Sh. 490 kwa kilo moja. Aidha, mkulima au kikundi kitakatwa kodi ya zuio asilimia mbili na mahindi yatafanyiwa ukaguzi wa ubora kabla  ya kuidhinishwa kupokewa”. AmeseMkurugenzi huyo.

Kuhusu malipo, Msigala amesema kuwa baada ya mahindi hayo kupelekwa ghalani malipo yatafanyika baada ya masaa 48. Mbali na hayo, Diwani wa Old Moshi Mashariki, Andrew Ringo ameeleza kuwa kwa vijiji vilivyopo ukanda wa milimani hususani Old Moshi, bei ya mahindi kwa gunia moja la kilo 100 itakuwa Sh. 75,000. Katika masoko ya mazao kama soko la Sadala Wilaya ya Hai na Sanya Juu katika wilaya ya Siha, gunia moja limefikia shilingi 80,000.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter