Home BIASHARA Kwanini kushirikiana ni tatizo kwa wengi?

Kwanini kushirikiana ni tatizo kwa wengi?

0 comment 107 views

Imekuwa ni kawaida kusikia kwamba ushirikiano huleta mafanikio zaidi. Lakini ni tofauti katika masuala ya kibiashara, biashara nyingi ambazo zimeanzishwa na mmiliki zaidi ya mmoja zimekufa kwa sababu wamiliki wa biashara hiyo wameshindwa kushirikiana ipasavyo ili kuleta maendeleo katika biashara yao.

Ikiwa kushirikiana kunaleta maendeleo katika biashara hivyo ni muhimu kwa wafanyabiashara kuzingatia haya ikiwa wanataka kufanikiwa katika biashara na kujipatia maendeleo:

Lengo la kuanzisha biashara na mtu mwingine siku zote huwa ni kufanikiwa zaidi hivyo ni muhimu kwa wote kuwa wakweli na kurekebishana pale mambo yakiwa hayaendi sawa. Uoga unaweza kusababisha biashara isiendelee. Hivyo ni muhimu kurekebishana, kuambiana ukweli inapobidi ili mambo yaende sawa, mawasiliano ni muhimu katika biashara.

Pia ni muhimu kupeana majukumu ili kuhakikisha mambo yanafanyika kwa muda uliopangwa. Si lazima wote mfanye jambo moja kwasababu ni wamiliki. Pia kupeana majukumu kutarahisisha swala la kuajiri,  kwani mkipeana majukumu kulingana na utaalamu kati ya wamiliki kutapunguza matumizi ya fedha kuwaajiri watu wengine.

Kupeana muda pia ni muhimu. Hivyo uvumilivu katika biashara ya kushirikiana ni muhimu. Kwasababu mkishajuana itakuwa ni rahisi kufanya kazi kwasabau kila mtu atajua ni kitu gani anakiweza zaidi, na kitu gani kinamshinda. Hivyo kuvumiliana ni swala la msingi sana katika biashara ya kushirikiana, lakini hiyo haimaanishi uvumilie mambo mabaya ambayo hayawezi kubadilika.

Vilevile itapendeza kama mtu unayeshirikiana naye katika biashara ana malengo yanayoendana na wewe. Sio lazima yaendane kwa asilimia miamoja. Lakini ni muhimu yakiendana zaidi katika maswala ya kazi ili wote muone kwamba mnafanya kazi kwa usawa na hakuna mtu ambaye anafanya kazi zaidi ya mwenzie. Hii itapelekea Amani katika biashara na malumbano yasiyo na msingi hayatokuwepo baina ya washirika katika biashara.

Mbali na hayo, washirika katika biashara wanashauriwa kusuluhisha changamoto katika biashara kwa kutumia mantiki na si hisia. Kutumia hisia kazini siku zote huleta matatizo zaidi. Hivyo ili kuendeleza biashara ni muhimu kutumia mantiki kusuluhisha changamoto zozote katika biashara ili kuleta maendeleo katika biashara na si kurudi nyuma.,

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter