Ikiwa unadhani unataka kukopa fedha, hakikisha unaweza kulipa malipo yoyote ya mwezi kila mwezi mbali na majukumu yako mengine. Kujua hasa fedha ambazo zinaingia na kutoka kila mwezi kutakusaidia kujua kama unaweza kumudu kukopa au la.
Weka bajeti. Njia pekee ya kujua kama unaweza kuazima fedha ni kuweka bajeti. Hii itakusaidia kujua kama kuna fedha yoyote inabaki mwisho wa mwezi baada ya kulipa bili zako zote na gharama za maisha
Vitu unavyotakiwa kujumuisha katika bajeti yako ni pamoja na: gesi, umeme, kodi ya maji, bima ya nyumba, mikopo iliyopo, bili ya TV, mafuta, kodi za gari, matengenezo ya gari, usafiri, mavazi, chakula, mambo mengine binafsi, kula nje, ununuzi wa magazeti, n.k. Tengeneza orodha kulingana na matumizi yako kwani sio kila nyumba ina matumizi sawa.
Ni wazo nzuri kukusanya akaunti ya benki na taarifa za kadi ya mkopo kutoka miezi mitatu iliyopita na kurekodi kila kitu unachotumia kwa muda wa mwezi au zaidi (kama unaweza kuwa na bili ambazo zinachukua miezi sita au kumi na mbili).
Hakikisha unajumuisha kila kitu unachotumia ili kupata picha ya kweli na kuepukana na mfumuko wa bei na gharama yoyote isizotarajiwa. Ukishajua tu, ni kiasi gani unahitaji kuweka na kiasi unachotumia kwa mwezi mmoja basi utaweza kuona kama unaweza kumudu deni lolote jipya.
Kagua ahadi ulizojiwekea kuhusu fedha, angalia kama kipato chako kinaweza kulipa mikopo na bili ikiwa siku umeanza kuumwa au umepoteza kazi. Kama unapata ugumu kulipa bili za mwezi na una mikopo mingi basi ni vizuri ukichunguza madeni yako na kuona ni jinsi gani unaweza kuyapunguza. Chochote utakachofanya epuka kulipa deni kwa fedha za mkopo.
Ikiwa bajeti yako inaonyesha kuwa una fedha za ziada zinazoweza kukuwezesha kukopa bado ni muhimu kuchukua muda wako kulinganisha maeneo mbalimbali ya mikopo ili kupata mkopo sahihi.
Kama bajeti yako haikuruhusu kukopa basi usikope zaidi kwasababu ukikopa itaonekana kuwa unajali tu hali yako ya sasa ya kifedha lakini hutilii maanani shida ilipo.
Tengeneza mpango ili uweze kuhakikisha unalipa deni lako.