Home VIWANDAUZALISHAJI Usiamke bila muelekeo, jipange

Usiamke bila muelekeo, jipange

0 comment 104 views

Siku zote unapojua ni nini unafanya na kwa sababu gani basi kuna jambo kubwa ambalo limejificha nalo si jingine bali ni faida. Siku zote mtu yoyote ambaye amejizatiti katika kujishughulisha na shughuli za kila siku ili mradi ni zenye manufaa kwa ajili yake na taifa basi mtu huyu tunamuweka katika kundi la watu wanaojitambua na wanajua nini wanafanya.

Haijalishi ni shughuli kubwa kiasi gani na inamuingizia kipato kiasi gani kikubwa tu ni kujua kuwa mtu huyu ana maono makubwa ya mbeleni au ana uwezo wa kujitimizia mahitaji yake ya kila siku.

Watu wengi wanaohusika na uzalishaji na shughuli za hapa na pale hasa katika nchi za Afrika wamekuwa wakishindwa kuendelea kwa sababu ya kukosa jambo muhimu la kuwafanya waweke nguvu kubwa katika shughuli zao za uzalishaji mali. Watu wengi wanakosa mipango madhubuti.

Hakuna jambo unaloweza ukafanikiwa kwa kiasi kikubwa bila kuwa na mipango. Watu wengi wamekuwa wakilala na kuamka bila kuwa na mipango au ratiba rasmi inayowaonyesha mlolongo wa shughuli nzima zitakavyoenda kwa siku hiyo. Wanabaki ni watu wa kuitwa huku na kule maana wanakosa ratiba yoyote inayowaongoza.

Leo ni vyema kuangalia umuhimu wa mtu kuamka akiwa na mipango ya siku au wiki sambamba na njia zitakazomsaidia kufanikiwa katika kutekeleza mikakati yake.

Kwanini unahitaji kuwa na mipango ya kila siku na kila wiki?

  1. Inasaidia kuondoa msongo wa mawazo kwa sababu utakuwa una mipango ambayo umeiweka ili kuitimiza kwa muda fulani itakupa utulivu wa akili na kutafuta njia bora za kukuamilisha mipango yako, huku ukiwa na uhakika kwa kutimiza mipango yako kwa asilimia kubwa
  2. Inasaidia kukabiliana na vikwazo na namna bora ya kuvitatua vikwazo hivyo. Mtu yoyote aliye na mipango katika suala zima la uzalishaji mali lazima awe na njia mbadala ya kuchukua tahadhari katika shughuli hiyo. Hii inamsaidia katika kujua namna anavyoweza kukabiliana na masuala mbalimbali yanayoweza kuwa kikwazo cha biashara yake kushuka ikiwa ni pamoja na suala la hasara , uvunjifu wa bidhaa, upotevu wa mali na hivyo kuwa na mbinu mbadala za kurudisha upya faida au mtaji wake pale unaposhuka.
  3. Inasaidia kukupa tathmini ya utendaji wako wa kazi. Ni ukweli usiopingika kuwa watu wasio kuwa na mipango na malengo hawana muda wa kufanya tathmini. Hii inatokana na ukweli kwamba hauwezi kufanya tathmini kwenye jambo ambalo haujalipanga. Mtu yoyote anayeweka malengo na mipango kwenye shughuli zake za kiuzalishaji lazima afanikiwe kwa sababu atakuwa na muda wa kujihoji endapo ameshuka au amepanda kulingana na muda aliopanga kukamilisha shughuli yake.

Hatua za kufuata ili kukamilisha mipango yako

  1. Ainisha malengo yako. Jaribu kutumia muda kidogo kuainisha malengo yako katika maandishi hii itakufanya kuwa makini na kufuata kile ulichokiandika kwa usahihi kuliko kuwa nacho katika kichwa chako maana kuna uwezekano wa kusahau baadhi ya mambo muhimu.
  2. Panga mikakati katika kutekeleza malengo yako. Panga kazi zote muhimu katika utaratibu wa kimantiki na kugawa muda uliohesabiwa wa kukamilika kwa kila lengo kwani itakuwa na manufaa wakati unapoanza ratiba ya shughuli hizi
  3. Jua njia utakazotumia/zitakazokusaidia kukamilisha malengo yako. Hii itakusaidia katika kufanikisha shughuli yako kwa sababu utaweza kujua ipi ni njia nzuri na ipi ni mbaya, sambamba na namna ya kuchukua tahadhari kwa njia utakazotumia kukamilisha malengo yako
  4. Panga muda wa kukamilisha malengo yako- Muda nui muhimu katika kukamilisha mipango. Muda unasaidia mtu kijitathmini endapo ametimiza kwa muda mwafaka, amewahi au amechelewa na hivyo kumpa wasaa wa kuweza kujua pale alipo. Kaa kwa muda mfupi kisha tahtmini kwa siku nzima uliyojishughulisha mipango yako ilienda ama ulivyopanga? Na je iliendana na uhalisia wa muda uliopanga kukamilisha?
  5. Tathmini utendaji wako wa kazi katika kukamilisha malengo yako na jinsi ufanikishaji wake ulivyokuwa. Je, ulikuwa wa kusuasua, au ulikamilisha kila jambo sawa na vile ulivyopanga liwe. Hii itakusaidia wakati mwingine kujua namna gani unapambana na changamoto zilizokufanya uchelewe au usifanikishe shughuli yako kwakiwango ulichokuwa unataka.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter