Home VIWANDAUZALISHAJI Tanzania kujifunza teknolojia magari ya umeme Singapore

Tanzania kujifunza teknolojia magari ya umeme Singapore

0 comment 56 views

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Tanzania inayo nafasi kubwa ya kujifunza Teknolojia ya uwambaji wa magari (Assembling) yanayotumia umeme kutoka kiwanda cha magari cha HYUNDAI kwani ni rafiki kwa mazingira na hupunguza uchafuzi wa hali ya hewa.

Dkt. Biteko ameyasema hayo Oktoba 23, 2024 nchini Singapore mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara mojawapo kwenye mkutano wa Wiki ya Nishati nchini Singapore na kusema kuwa Teknolojia kama hizo zina mchango mkubwa kwenye kuinua uchumi wa nchi na kuongeza pato la Taifa.

“Nawapongeza sana wenzetu hasa kwa Teknolojia na ubunifu wa haya magari pamoja na Teknolojia ya Kilimo janja (smart farm) ambapo kwanza inatumia nafasi ndogo lakini matokeo yake ni makubwa sana,’’ amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko ashuhudia teknolojia ya kilimo janja (Smart farm) kinachotumia Teknolojia Mnemba

Kuhusu Teknolojia ya kilimo janja ambacho kinaendeshwa na kampuni ya ubunifu ya HYUNDAI kwa kutumia Teknolojia mnemba (Robot) Dkt. Biteko amesema, uwepo wa Teknolojia kama hii unaongeza tija, inapunguza gharama kwenye uendeshaji wake.

Naye, Makamu wa rais na Mkuu wa Biashara na mipango kutoka HYUNDAI Motor Group amesema mafanikio hayo yanayokana na kutumia fursa iliyopo wakati wa changamoto zilizokuwepo awali kama ya matumizi ya mafuta kwenye magari ambapo haikuwa rafiki kwa mazingira pamoja na uhaba wa maeneo kwa ajili ya kilimo nchini Singapore.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter