Home BIASHARA Unataka mafanikio ndani ya muda mfupi?

Unataka mafanikio ndani ya muda mfupi?

0 comment 134 views

Kila mfanyabiashara hutaka kila kitu katika biashara yake kiende sawa. Muda ni mali lakini katika biashara uwezo wa kufanya majukumu mengi katika muda mchache ni muhimu zaidi. Hata wafanyabiashara waliofanikiwa wamekuwa wakijali sana matokeo ya kazi wanazofanya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila kitu kinafanyika katika muda mchache.

Ni muhimu kwa wajasiriamali kuanza kuzingatia zaidi matokeo ya kazi yanayofanyika katika muda mchache ili kuweza kufanikiwa.

Mwaka 1926 mwanzilishi wa kampuni ya Ford, Henry Ford alifanya uchunguzi na kugundua kuwa ikiwa mtu atapunguza muda wake wa kila siku wa kufanya kazi kutoka masaa 10 hadi nane na kufanya kazi siku tano badala ya sita basi hata uzalishaji wake utaongezeka. Ni muhimu kujiwekea muda ambao ni rafiki kwako kwa ajili ya kazi na katika muda ambao unakuwa na majukumu ya kufanya jitahidi kutumia muda mchache kwenye mambo yasiyokuwa na umuhimu kwako na kwa biashara yako kwa mfano kutumia mitandao ya jamii ili hali majukumu uliyonayo hayaruhusu. Pia, jifunze kusema hapana pale inapobidi.

Aidha, ni muhimu kujua mambo ya kufanya zaidi, ikiwa ni pamoja na kujiwekea muda maalum wa kumaliza kazi. Gawa majukumu mengine ili kuyafanyia kazi kwa juhudi mambo muhimu ambayo una ujuzi nayo. Fanya zaidi kazi zinazoongeza mapato na wateja, tengeneza mfumo katika biashara yako. jitahidi kuwa na muda wa kupumzika ili akili iweze kuongeza ufanisi pale utakapoendelea na kazi na mwisho wa siku andika mambo ya kufanya kesho ili kuitayarisha akili yako.

Ni muhimu kuangalia mambo ya msingi na kuhakikisha yanafanyika kama inavyostahili. Kabla ya kufanya jambo husika jitahidi kujua kama kuna umuhimu wa kulifanya wewe mwenyewe jambo hilo au unaweza kumpa mwingine kazi hiyo na kuendelea na mambo yenye umuhimu zaidi.

Vilevile, kuwa na orodha ya vitu vya kufanya kulingana na aina ya biashara. Hii yote itarahisisha mafanikio yako ikiwa ni pamoja na kujua wateja wako, mambo yanayowavutia, nini cha kufanya ili kuwavutia zaidi, sababu zilizosababisha wateja wa kudumu kutafuta bidhaa sehemu nyingine na nini cha kufanya ili kubadilisha hilo na mambo mengine kulingana na biashara yako.

Jitahidi kujipa majukumu machache ili uweze kuyafanyia kazi na kufikia malengo. Biashara au kampuni zilizofanikiwa zimetengeneza mfumo na kuhakikisha kila mtu ana majukumu yake katika ofisi na anayatekeleza ipasavyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter