Home FEDHA Unapata akiba zaidi ukijilipa

Unapata akiba zaidi ukijilipa

0 comment 80 views

Watu wengi hawana desturi ya kujilipa katika mapato wanayopata kwa sababu wamejiwekea kuwa, fedha hizo ni za kwao hivyo ni sawa kuwalipa watu wengine na wao watanufaika kwa namna moja au nyingine. Kutumia fedha zako sio vibaya lakini kama huweki akiba ya kutosha ni muhimu kutafakari nini unafanya sasa.

Ni muhimu kutenga fedha kwa ajili ya gharama za matumizi ya kila mwezi lakini jambo la muhimu zaidi ni kujilipa kwa kufanya kazi. Jaribu kujilipa kila mwezi na kuelekeza fedha hizo moja kwa moja katika akiba. Kwa mfano kama una mkopo na unataka kulipa mkopo huo basi jitahidi kuwa na kiasi kadhaa kila mwezi na kuelekeza fedha hizo katika mkopo hadi utakapoisha na kisha angalia malengo unayotaka kutimiza na kisha wekeza katika malengo hayo. Baada ya muda utaona mabadiliko katika mtiririko wa fedha zako.

Kujilipa mshahara kabla ya kugawanya fedha zako katika matumizi mbalimbali kutasaidia kutumia fedha kwa nidhamu. Baada ya kujilipa utabaki na kiasi cha fedha ambacho utatakiwa kukiwekea bajeti na kutumia katika masuala ya msingi: hivyo kuelekeza fedha zako katika mambo muhimu

Watu wengi wana desturi ya kuweka akiba fedha zinazokuwa zimebaki baada ya kuelekeza fedha zao katika matumizi mbalimbali. Lakini unapojilipa kwanza mshahara kabla ya kuweka fedha katika matumizi mbalimbali inakusaidia kufikiria siku zijazo na kuweka kipaumbele katika malengo muhimu.

Njia rahisi ya kujilipa ni kujua kiasi ambacho unaweka akiba kwa sasa na kiasi unachotumia kwa mwezi. Anza kuwa makini katika matumizi yako ili kujua ni yapi hayana umuhimu ili uyatoe katika bajeti yako. Baada ya hapo fanya mahesabu kiasi cha fedha ambacho unatakiwa kuwa unawekeza kila mwezi- huo ndio utakuwa mshahara wako. Kurahisisha hili ni vyema ukawa unafanya muamala moja kwa moja (automatically) ili kuepuka kutumia fedha hizo. Kama unalipwa kwa benki, basi kila mwezi jitahidi kuweka fedha katika akaunti yako ya akiba moja kwa moja. Baada ya hapo unaweza kuendelea na gharama za matumizi mengine kama kawaida.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter