Home BIASHARA Siri ya huduma bora kwa wateja hii hapa

Siri ya huduma bora kwa wateja hii hapa

0 comment 153 views

Huduma bora kwa wateja ni muhimu kwani inatoa picha halisi ya ukuaji wa biashara yako. Hakuna biashara pasipo uwepo wa wateja hivyo kama unataka kufika mbali zaidi, ni lazima kuwekeza katika kuwapa wateja wako huduma bora zaidi ili kuwahamasisha kurudi tena na tena. Endapo unakwama katika kufanikisha hili, makala hii inakupa siri ya kuwahudumia vyema wateja wako na kuhakikisha kuwa biashara yako inatimiza malengo.

1. Sikiliza maoni na yafanyie kaziwateja

Maoni na ushauri kutoka kwa wateja ni nguzo muhimu katika maendeleo ya biashara hivyo hakikisha unasikiliza maoni haya na usiishie hapo tu, chukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa unayatekeleza. Wateja wanapoona kuwa mawazo yao yana thamani na wanasikilizwa, wanapata hamasa ya kuendelea kuwa wateja hivyo kuimarisha biashara.

2. Hakikisha kila mtu anafahamu bidhaa/huduma kwa undani

Ikiwa unaendesha biashara ambayo imeajiri wafanyakazi, basi ni vyema kuhakikisha kuwa kila mmoja wao ana uelewa wa kutosha kuhusu bidhaa au huduma inayotolewa kwani inapotokea mteja anahitaji ufafanuzi kuhusu suala fulani, inakuwa rahisi kupata majibu kwa haraka pasipo kuwa na usumbufu wowote.

3. Ajiri watu sahihi

Kuajiri watu wenye vigezo sahihi ni muhimu sana. Wateja wako wanategemea kupata majibu sahihi, kupata maelekezo husika pale wanaposhindwa kuelewa kitu fulani lakini kikubwa zaidi wanategemea kuwa wanasikilizwa na watu ambao ni wasikilizaji wazuri ambao wanaelewa changamoto zao.

4. Thamini watu kuliko faida

Badala ya kuwa na mawazo ya kutengeneza fedha pekee, sikiliza wateja wako na fahamu wanachohitaji. Waonyeshe kuwa unajali na kwamba bila wao biashara yako isingeweza kufika mahali hapo. Jifunze kuwa kuwa msikilizaji na wekeza katika kutoa huduma bora zaidi kwani ukifanya hivyo,

5. Fahamu wateja wako wanataka nini

Njia bora zaidi ya kuwa na wateja wa kudumu ni kugundua ni nini hasa wanataka kabla yao na kisha kutoa bidhaa au huduma hiyo kwa kiwango cha juu kabisa. Hii inasaidia kutengeneza mahusiano ya muda mrefu ambayo yanatokana na ukweli pamoja na uaminifu. Kama umewahakikishia wateja wako kuwa utafanya kitu, hakikisha unakifanya.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter