Home KILIMO Faida za maonyesho ya kilimo

Faida za maonyesho ya kilimo

0 comment 138 views

Ni dhahiri kuwa 70% ya watanzania ni wakulima na wengi wao ni wakulima wadogo. Michakato mbalimbali imekuwa ikiendelea kufanywa na serikali pamoja na sekta binafsi ili kuwainua wakulima na kukuza sekta ya kilimo kwani inayotegemewa na watanzania pia ina fursa nyingi ambazo zinaweza kuwanufaisha watu wengi hususani viana.

Katika harakati za kuendeleza sekta ya kilimo, kila mwaka huwa kuna maonyesho ambayo hufanyika kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 8 mwezi Agosti . Maonyesho hayo hufanyika kwanza kwa ajili ya kusherekea wakulima wote kutokana na mchango wao katika kuinua uchumi wa nchi, pia maonyesho hayo hufanyika ili kuelimisha, kuonyesha teknolojia na uvumbuzi mpya.

Kama mkulima, ni muhimu kuhudhuria katika maonyesho haya kwa sababu zifuatazo:

Mafunzo kuhusu teknolojia mpya

Mara nyingi katika maonyesho ya kilimo huwa kunakuwa na kampuni na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na teknolojia hivyo wakati wa maonyesho hayo hupeleka teknolojia mbalimbali za kisasa ili kuwaonyesha wakulima na watu ambao hufika katika maonyesho hayo. Kwa mkulima hiyo ni fursa kubwa kujifunza na kupitia mafunzo hayo unaweza nafasi ya kujua kama unaweza kumudu gharama au la. Baada ya hapo mkulima anaweza kujipanga na kuweza kumiliki teknolojia inayofaa katika shughuli zake ili kurahisisha mambo na kupata mazao zaidi.

Kutangaza bidhaa

Wakulima sio watu pekee wanaohudhuria maonyesho haya. Watu wa kawaida pia wanakuwepo hivyo kama mkulima unaweza kupeleka bidhaa zako na kuzitangaza kwa watu mbalimbali. Hii itakuza soko la bidhaa zako na kukuza idadi ya wateja hasa kama bidhaa zako zina kiwango kizuri na zinavutia. Ni muhimu kujua utaratibu wa kupata sehemu ili kuweza kutangaza biashara yako katika siku zilizotengwa kwa ajili ya maonyesho.

Mtandao

Kupitia maonyesho watu mbalimbali hukutana na kuwasiliana, kama mkulima mwenye malengo hili ni jambo zuri kwako kwa sababu unapata nafasi ya kukutana na watu ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako na pia unaweza kujitengenezea mtandao mpya wa wateja. Ni muhimu kuongea na watu tofauti, kujua mambo wanayojihusisha nayo. Lengo la maonyesho ni kuwaunganisha watu ili waweze kushirikiana katika masuala ambayo yataleta maendele.

Kutangaza bidhaa mpya

Kama ndiyo kwanza umeanzisha bidhaa mpya, maonyesho haya ni mahali pazuri kwa ajili ya kujitangaza. Hakikisha unatumia lugha nzuri kuwaelekeza watu kuhusu bidhaa hiyo, pia kama kuna uwezo wa kuijaribu bidhaa hiyo basi tengeneza namna ya kufanya hivyo.

Kujifunza

Ni muhimu kujua jinsi wakulima wengine wanafanya shughuli zao. Hapa unaweza kutazama tu pia unaweza kuuliza maswali kwa kufanya hivyo utaweza kugundua kuwa kuna mambo mengi ambayo ulikuwa huna ujuzi au uelewa nayo. Kwa namna moja au nyingine mtu yeyote anayehudhuria maonyesho lazima ataondoka na mafunzo na uelewa mpya.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter