Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Ubunifu wa mavazi unavyomlipa Wolper

Ubunifu wa mavazi unavyomlipa Wolper

0 comment 155 views

Ukizungumzia tasnia ya mitindo nchini, lazima umzungumzie mwanamitindo na msanii Jacqueline Wolper Massawe, maarufu kama Wolperstylish. Msanii huyo mwenye wafuatiliaji (followers) wapatao milioni 4.7 kwenye mtandao wa Instagram pekee ni miongoni mwa wanamitindo ambao wamekuwa wakijaribu kuinua tasnia ya mitindo kwa muda mrefu sasa baada ya tasnia hiyo kutokuwa inafanya vizuri hapo nyuma.

Mbali na usanii, Wolper anamiliki kampuni ya ‘House of Stylish’ ambayo inahusika na ubunifu wa nguo na amekuwa akibuni mavazi ambayo watu wengi wamekuwa wakishangazwa nayo. Mjasiriamali huyo amekuwa akatangaza biashara yake kwa kuvaa nguo zake mwenyewe ili kuwahamasisha wateja kununua.

Msanii huyo amekuwa akisikika mara kadhaa kuwa anataka kuwasaidia watu hasa wanawake kujiajiri na kuacha kutegemea fedha kutoka kwa wanaume. Pia kutokana na umaarufu wake itakuwa rahisi kuwasaidia watu wengine wenye vipaji kutangaza bidhaa zao na kujipatia kipato au kupata msaada kwa watu wenye uwezo zaidi kwa kuwekeza fedha na kuwapeleka katika mafanikio.

Aidha, kutokana na mavazi anayobuni kuwa ya tofauti, Jacqueline Wolper ana ndoto ya kuwavalisha watu maarufu duniani kama Rihanna na Beyonce.

Ni muhimu kwa vijana kujifunza kutoka kwa mwanamitindo huyu, ambaye anaamini kuwa anaweza kufanya mabadiliko makubwa kupitia kipaji chake. Muda umefika kwa vijana kuacha kuchagua kazi za kufanya wakihofia jamii itakavyowachukulia kwa sababu mafanikio hupatikana popote ikiwa una bidii, ujasiri na uvumilivu pale mambo yasipokwenda sawa, pia kujua unataka kujihusisha na wateja wa namna gani ili kuhakikisha unakuwa na soko la uhakika.

Siku zote inashauriwa kufanya mambo ambayo unafurahia ili kuweza kuyafanya kwa juhudi na urahisi. Kama unatumia nguvu kubwa na hufurahii kile unachokifanya ni vyema kujitafakari. Usisubiri kufanya mabadiliko kwa sababu hakuna wakati muafaka wa kufanya hivyo.

Anza leo na ishi ndoto zako..

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter