Home BIASHARA Migahawa isipotoshe wateja mtandaoni

Migahawa isipotoshe wateja mtandaoni

0 comment 126 views

Mitandao ya kijamii imekuwa na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara hususani wafanyabiashara wa vyakula. Wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mitandao kujipatia wateja zaidi. Kwa baadhi ya wafanyabiashara mitandao ya kijamii imewasaidia kupata mafanikio makubwa huku wengine wakipata changamoto ya kupoteza wateja kutokana na kuweka picha na video ambazo haziendani na hali halisi na vilevile kutoa huduma mbovu.

Kwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri, ni rahisi kujulikana zaidi na kukuza biashara. Wateja wanapotumia bidhaa na kuzifurahia wanahamasika kutangaza biashara yako kwa mfano kwa kuweka picha au video za chakula chako kwenye kurasa zao hivyo kuhamasisha watu wengine kufuatilia na kununua chakula chako kitu ambacho ni kizuri katika biashara.

Hakuna mmiliki wa biashara asiyefurahishwa na mrejesho mzuri wa huduma anazotoa. Ikiwa kile unachoweka mitandaoni ndiyo kile watu hupata ni rahisi kupata mrejesho mzuri na kuhamasisha wateja zaidi kutumia bidhaa na huduma zako.

Hata baada ya kupata umaarufu, mrejesho mbaya kutoka kwa wateja utaathiri mtiririko wako wa fedha katika biashara kwa sababu hakuna mtu ambaye hutaka kununua chakula sehemu ambayo anajua hatoridhika.

Kama mfanyabiashara ni vyema kukumbuka malengo yako kila wakati ili kujua wapi ulipotoka na wapi unakwenda, kwa kuwa sio kila siku mambo yatakua mazuri katika biashara hivyo hakikisha mtiririko wako wa fedha unaenda sawa kwa kutoa huduma bora ili kuepuka kukosa wateja.

Baadhi ya sehemu ambazo zinasifika kwa chakula na huduma nzuri kwa ujumla jijini Dar es salaam ni pamoja na Club Afrikando, Chef Kile, Open Kitchen, Lin BBQ  na Etina Restaurant iliyopo eneo la Survey.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter