Home FEDHA Jinsi ya kupata mtaji wa biashara

Jinsi ya kupata mtaji wa biashara

0 comment 131 views

Mitaji imekuwa kikwazo kwa wafanyabiashara walio wengi. Asilimia kubwa wanapata wakati mgumu kuendeleza mawazo waliyonayo kutokana na kukosa fedha kwa ajili ya kuanzisha biashara wanazotaka. Kuna mbinu ambazo unaweza kutumia ili kupata kiasi kidogo tu cha fedha ambacho kitakuwezesha kuanzisha biashara yako. Ingawa mtaji sio kigezo pekee cha kufanikiwa katika biashara, fedha ni kiungo muhimu katika kutekeleza wazo au mradi kwa ufanisi.

Ikiwa unapata wakati mgumu katika kupata mtaji kwa ajili ya biashara yako, unaweza kufanya yafuatayo ili kuendeleza wazo lako:

Akiba: Kuna faida mbalimbali za kujenga mazoea ya kuweka akiba. Ikiwa una fedha kidogo za akiba inakuwa rahisi kuzitumia kama mtaji pale ambapo upo tayari kuanzisha biashara. Akiba inakuwezesha kuchangamkia fursa na kuzifanyia kazi kwa wakati. Hivyo, unaweza kutunza kiasi fulani cha fedha hata kama ni kidogo, ili kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako. Inashauriwa usianze biashara na mtaji mkubwa sana kwani unaweza kupata hasara. Usitumie akiba yako yote kwa wakati moja kama ndiyo kwanza unaanza biashara.

Marafiki na Familia: Kama una mahusiano mazuri na ndugu zako, unakuwa katika nafasi nzuri ya kuandaa wazo lako la biashara n kuwaomba wakusaidie kupata mtaji ili kuendeleza wazo hilo. Mara nyingi mikopo ya aina hii baina ya ndugu haina riba, masharti wala vikwazo vya aina yoyote hivyo inakuwa rahisi zaidi kupata. Jambo la muhimu ni kuwa muaminifu na kurejesha fedha ulizopatiwa ndani ya muda mliokubaliana.

Taasisi za ujasiriamali: Leo hii kuna taasisi na mashirika mbalimbali yanayotoa mitaji kwa wajasiriamali  ili kuwawezesha kutimiza malengo yao. Baadhi ya taasisi hizo ni pamoja na Small Starter, Iesc na Afrika Connekt. Hakikisha unafuatilia katika vyombo ya habari pamoja na mitandao ya kijamii au vikundi vya wajasiriamali ili zinapotokea fursa upate kuzifahamu na kuzitumia ipasavyo.

Taasisi za fedha: Mikopo kutoka taasisi za fedha inaweza kuwa mtaji mzuri wa biashara. Kama unataka kupata mtaji kwa njia hii, hakikisha umejipanga vizuri na unafahamu mbinu utakazotumia kurejesha mkopo huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter